
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
Mahakama ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela Saidi Saidi Chalamanda (49), mkazi wa Kijiji cha Fundimbaga, baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki pombe haramu aina ya gongo.
Hukumu hiyo ilisomwa Aprili 14, 2026 na Hakimu wa Mahakama hiyo, S.J. Mwampashe, kufuatia ushahidi uliowasilishwa mahakamani kuthibitisha kosa hilo pasipo shaka.
Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, mtuhumiwa alikamatwa Machi 19, 2026 katika Kijiji cha Fundimbaga, wilayani Tunduru, akiwa na lita 4.5 za pombe haramu ya moshi (gongo). Baadaye alifikishwa mahakamani Aprili 14, 2026 kujibu shtaka hilo.
Mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa huyo chini ya Kifungu cha 30 cha Sheria ya Udhibiti wa Vileo, Sura ya 384 (marejeo ya mwaka 2023), kinachokataza umiliki na usambazaji wa pombe haramu.
Leave a comment