Na Damasi Kalembwe

Mkaguzi wa Polisi wa Kata ya Kijitonyama, INSP Kavula Mizeye, ametoa mafunzo kuhusu maadili, malezi bora na kupinga ukatili wa kijinsia kwa vijana na watoto 39 waliokusanyika katika Uwanja wa Mpira wa Vinyago, uliopo Mtaa wa Nzasa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, INSP Mizeye alisema lengo ni kuwajenga vijana katika misingi bora ya maadili na malezi, huku akiwahimiza kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya, vitendo vya ukatili wa kijinsia, ikiwemo ubakaji, pamoja na kuachana na makundi ya kihalifu yanayoweza kuhatarisha usalama wao na wa jamii.

Aidha, aliwataka vijana hao kuwa mabalozi wa amani na usalama kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia utoaji wa taarifa za siri na za kiintelijensia kuhusu viashiria au uwepo wa wahalifu katika maeneo yao, ili kusaidia kuzuia na kupambana na uhalifu.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Bw. Gervaz Nabyasinu alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatia elimu hiyo, akisema imewajengea uelewa kuhusu wajibu wao katika kudumisha amani na usalama.

Alihaidi kuwa vijana hao watashirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi katika kufichua na kupambana na vitendo vya kihalifu vinavyoweza kujitokeza katika jamii.

Posted in

Leave a comment