Category: Uncategorized

  • Na Abel Mwakingwe Wananchi wa Makunganya, Morogoro, sasa wana unafuu wa upatikanaji wa maji safi na salama baada ya kisima chenye thamani ya Shilingi milioni 38 kukabidhiwa kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya matumizi ya jamii na shughuli za uhifadhi. Kisima hicho, kilichotolewa na Mkwawa Group of Campaign na kukabidhiwa…

  • Na Andrea Mlwafu Kila msimu wa mavuno, Tanzania huacha nyuma yake kiasi kikubwa cha mabaki ya kilimo—maganda ya mpunga na mihogo, magunzi na mabua ya mahindi, masalia ya pamba, miwa, kahawa na mazao mengine. Kwa macho ya wengi, hayo ni taka zinazopaswa kuondolewa. Lakini kwa wajasiriamali na wabunifu wa teknolojia, yanaweza kuwa malighafi ya biashara…

  • Na Pilastus Nyaulingo Kilimo Tanzania kinaingia katika hatua mpya, ambapo akili bandia (AI), teknolojia za simu na mifumo ya kidijitali vinaanza kubadili namna wakulima wanavyopata masoko, pembejeo, huduma za fedha na taarifa za uzalishaji, huku vijana wakitumia ujuzi wao kuibua biashara na suluhisho mpya ndani ya sekta hiyo. Mabadiliko hayo yanaibua fursa kwa vijana wenye…

  • Na Abel Mwakingwe Wananchi wa Wilaya ya Nkansi na Manispaa ya Sumbawanga wanatarajiwa kupata huduma bora zaidi za afya baada ya Zahanati za Chala na King’ombe kupatiwa vifaa tiba vyenye thamani ya jumla ya Sh milioni 312. Zahanati ya Chala imepokea vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 267, huku Zahanati ya King’ombe katika Manispaa ya…

  • Na Iddy Mziray, Songea Wazee mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuhakikisha haki zao zinatekelezwa, ikiwamo kupata matibabu bure na kipaumbele hospitalini, kulipwa pensheni kwa wakati na kulindwa dhidi ya unyanyasaji. Wazee hao walitoa kilio hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika Kata ya Lizaboni, Songea, ambapo walifanya maandamano mafupi kutoka Shule ya Msingi…

  • Na Cartace Ngajiro – Tanga Uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Tanga umeongeza shughuli za bandari hiyo na kufungua fursa mbalimbali kwa wananchi, huku ukichangia kukuza mnyororo wa thamani na kuongeza mchango wa bandari katika maendeleo ya Mkoa wa Tanga na taifa kwa ujumla. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Almas Nyangasa, wakati…

  • Na Grace Mwakalinga WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametakiwa kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro wa madereva wa mabasi na malori, huku akitakiwa kuitisha mazungumzo na wadau wa sekta hiyo ili kurejesha huduma za usafiri nchini. Wito huo umetolewa na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani wa ACT Wazalendo, Naggy Kaboyoka,…

  • Na Grace Mwakalinga CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai kimepanga kuitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili sakata la Mwenyekiti wa CCM Kata ya Bomang’ombe, Agness Kimaro, aliyedai kuwekwa ndani kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Hassan Bomboko. Kimaro alikamatwa Septemba 25, 2026, wakati akielekea kwenye shughuli za ujenzi wa shina la…

  • Na Iddy Mziray, Songea Madereva wa mabasi ya abiria mkoani Ruvuma wameendelea na huduma ya usafirishaji baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa huo, SACP Marco Chilya, kuwahakikishia ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi. Chilya alitoa kauli hiyo jana alipokutana na madereva, abiria, wananchi na wadau wa usafirishaji katika Stendi ya Mabasi iliyopo Kata…