Category: Uncategorized
-
Na Cosmas Msuha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema katika mwaka wa fedha 2026/27 inatarajia kuajiri watumishi wapya 10,919 pamoja na kutekeleza vipaumbele vinane vinavyolenga kuimarisha usalama, huduma za uraia na matumizi ya teknolojia nchini. Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma Mei 25, 2026, Waziri wa Mambo…
-
Na Cosmas Msuha Shughuli za uchimbaji madini katika Mgodi wa Namungo uliopo Wilaya ya Ruangwa zimeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa eneo hilo, huku wachimbaji waliokuwa wakihangaika kimaisha wakianza kunufaika na maendeleo kupitia sekta ya madini. Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Lindi, Dickson Joram alisema shughuli za…
-
Na Cosmas Msuha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Msalato Satellite City unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) katika eneo la Msalato jijini Dodoma. Ziara hiyo ya ukaguzi ililenga kujionea…
-
Na Mwandishi Wetu, Songea Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma limeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Good Shepherd Montessori iliyopo Mjimwema, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Elimu hiyo ilitolewa na watendaji wa Dawati la Elimu kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa…
-
Na Cartace Ngajiro, Tanga Serikali ya Jamhuri ya Rwanda imesema itaendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Bandari ya Tanga pamoja na kuendelea kutumia bandari hiyo kupitishia mizigo yake. Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba, alipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa bandari…
-
Na Cosmas Msuha WOMESA imewataka wanawake kutumia fursa mbalimbali za ajira zinazopatikana katika sekta ya bahari, ambazo zinagusa nyanja tofauti za kijamii na kiuchumi. Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa TASAC, Mwatano Maganga, wakati wa kongamano la maadhimisho ya umoja huo lililofanyika Bagamoyo, mkoani Pwani. Maganga alisema sekta ya…
-
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma Wananchi wa Kijiji cha Maposeni wametakiwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na wageni wanaowatia shaka katika maeneo yao ili kudhibiti matukio ya uhalifu. Kauli hiyo ilitolewa na Polisi Kata wa Maposeni, Mkaguzi wa Polisi (Insp.) Ramadhani Duru, alipokuwa akizungumza na wananchi hao huku akisisitiza umuhimu wa…
-
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama pamoja na matumizi sahihi ya elimu, vipaji na ubunifu wa vijana katika kudumisha amani, mshikamano na maendeleo ya jamii. Wito huo umetolewa Mei 8, 2026 na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Ruvuma,…
-
Na Mwandishi Wetu, Songea Wamiliki wa kampuni za ulinzi mkoani Ruvuma wametakiwa kuhakikisha wanasimamia ipasavyo na kulipa stahiki za askari wao kwa wakati, ili kuwaepusha na vitendo vya uhalifu kama vile wizi wa mali za wananchi pamoja na kuchukua mikopo yenye riba kubwa inayosababisha kukosa uadilifu kazini. Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Polisi Jamii…
-
Na Cosmas Msuha Tume ya Madini, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), inaendelea kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo nchini ili kuboresha ujuzi wao na kuongeza tija katika sekta ya madini na uendelezaji wa Taasisi ya Uchimbaji Mdogo wa Madini (FADev). Akizungumza na wananchi Aprili 19, 2026 mkoani Morogoro, mwakilishi wa…